All Sermons
Bible Passage Luka 3:9
This content is part of a series Daily Bread, Salvation, in topic Holiness & book Bible.

SAFARI YA MTENDA DHAMBI

  • Addo November Mwasongwe
Date preached July 4, 2019

Nikiwa bado ni mwanafunzi wa Imani bado Nina wajibu wa kuueleza umma kile ambacho ninasikia ndani yangu Mungu Akinisemesha ili nisijedaiwa.

Nimepoteza marafiki zangu ambao nilikua nasema nitamwambia ukweli kesho mara paap wameshakufa, wiki mbili zilopita rafiki yangu sana Eze amefariki nilikua naye namchukulia poa namuhubiria kishkaji asikwazike.

Sasa nimeamua kuwa wa kizamani ambaye nimepitwa na wakati bora ujumbe ufike sasa hata kama watachukia no sweat tutapongezana Mbinguni.

Haya kwa wale wanaotaka Kumwimbia Mungu na bado wako dhambini Neno la Mungu Linasema
Zaburi 150:6
Kila mwenye pumzi na amsifu BWANA. Haleluya.

Msimamo mwingine ni huu hapa
Zaburi 33:1
Mpigieni BWANA vigelegele, enyi wenye haki, Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo. Pigia Mstari Wanyofu wa Moyo.

Je wewe unayesema haina shida kumsifu Mungu Ukiwa dhambini je ni mnyoofu wa moyo?

2 Timotheo 2:19

Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu.

Jiulize wewe unayejisnap kila Saa na nyimbo za Mungu zenye Kumtaja Mungu Yesu Kristo Umeuacha Uovu? Usijiongezee dhambi ulizonazo zinakutosha

Je unajua ya kuwa unajifurahisha tu maana Mungu Hawasikii wenye dhambi

Soma Yohana 9:31
Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo.

Namalizia kwa kusema Tubu sasa uanze ku enjoy Luka 5:32
Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi, wapate kutubu.
Siku zimeisha Yesu Amekaribia KURUDI
Luka 3:9
Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni.

Unakoelekea ni Mbinguni au Motoni hakuna mitaa ya katikati chagua leo.

Amua leo. Kutubu ni Kugeuka Kutubu ni kuacha kutubu ni Kujutia ni Mwanzo mpya inaanza na wewe mpendwa wangu.

 

In series Daily Bread